KIMBUNGA HIDAYA CHAZIDI KUIMARIKA, HII HAPA TAARIFA MPYA KUTOKA TMA

03/09/2026 · Mwananchi Digital

Descrição

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) leo Ijumaa, Mei 3, 2024 saa 3:00 asubuhi imetoa taarifa ya kuimarika na kuendelea kusogea kwa Kimbunga Hidaya katika pwani ya Bahari ya Hindi. “Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga “HIDAYA” kilichopo katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya nchi yetu. “Kimbunga “HIDAYA” kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo hadi kufika saa tisa usiku wa tarehe 03 Mei 2024 kilikuwa kimeimarika zaidi na kufikia hadhi ya kimbunga kamili, kikiwa umbali wa takriban kilomita 401 mashariki mwa pwani ya Mtwara. “Katika kipindi hiki, Kimbunga HIDAYA kimeendelea kuimarika zaidi huku kasi ya upepo ikiongezeka hadi kufikia kilomita 130 kwa saa,”imesema taarifa hiyo. Taarifa kuhusu matarajio ya kimbunga Hidaya, zilianza kutolewa jana Alhamisi Mei 2, 2024 na TMA ilisema kingekuwa na nguvu ya kati katika umbali wa kilomita 506 mashariki mwa Pwani ya Mtwara. TMA ilitaja mikoa hiyo inaweza kukumbwa na kimbunga hicho kuwa ni Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Visiwa vya Unguja na Pemba na maeneo mengine ya jirani. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mwenendo wa mfumo wa hali ya hewa baharini ulionyesha uwezekano wa kimbunga hicho kusogea karibu na Pwani ya Tanzania kuanzia usiku wa Mei 2, 2024 na kuendelea hadi Mei 6, 2024. Kimbunga hicho, kinatazamiwa kuwa kikubwa zaidi kuwahi kutokea nchini. (Imeandikwa na Mwandishi Wetu) #samiasuluhuhassan #simbasc #yangasc #mashabiki #nbcpremeireleague #cafchampionsleague #cafconfiderationcup #ikulumawasiliano #entertainment #music #news #yangasc #simbasc #cafchampionsleague #mayele #highlights #cafconfiderationcup #riversunited #mashabiki #yangaleo #yanga #timuyawananchi #daimambelenyumamwiko #entertainment #music #news #magoliyasimba #magoliyayanga #magoliyote #magoliyamayele #mayele #aziziki #manara #manaraleo #ikulumawasiliano #magufuli #kikwete #mayele #singidabigstars #magoliyamayele #magoliyasimba #magoliyayanga #highlights #azamsportsfederationcup #chama #Shot #mamelodisundowns #alahlytv #alahlysc #miraj

Palavra-chave: meteorologia pemba

Tags: Mwananchi · Thecitizen · Mwanaspoti · MCL · Tanzania News · Tanzania makutukio · Habari Tanzania events · wema · Magufuli

Comentários