HABARI : TMA YATOA TAHADHARI YA VIPINDI VYA MVUA KUBWA.

01/09/2026 · open online media

Descrição

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari juu ya uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, maeneo yanayotarajiwa kupata mvua kubwa ni mikoa ya Geita, Kagera, Shinyanga, Kilimanjaro, Arusha, Singida, Mwanza, Simiyu, Mara na Manyara pamoja na Tanga na visiwa vya Unguja na Pemba. TMA imesema maeneo mengi nchini yanaendelea kupata mvua kutokana na hali ya hewa ilivyo kwa sasa, hivyo wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari hususan katika maeneo yenye miinuko, mabondeni na karibu na mito. Open Online Media itaendelea kukuletea taarifa za hali ya hewa na tahadhari muhimu kwa wananchi. Tuachie maoni yako. #pakua app ya Open Media kupata habari na kusikiliza Open Online Radio #follow, comment na ku like post za Open Online Media ili uwe wa kwanza kupata habari

Palavra-chave: meteorologia pemba

Tags: Utabiri wa hali ya hewa · Weather Forecast