HABARI : TMA YATOA ANGALIZO LA VIPINDI VYA MVUA KUBWA BAADHI YA MAENEO NCHINI.
Descrição
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la uwezekano wa vipindi vifupi vya mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini.
Kwa mujibu wa utabiri wa mamlaka hiyo, mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba vinatarajiwa kupata mvua kubwa katika baadhi ya maeneo.
TMA imewataka wakazi wa maeneo hayo kuchukua tahadhari hususan katika maeneo ya mabondeni na karibu na mito kwani kuna uwezekano wa baadhi ya makazi kuzungukwa na maji.
Aidha, mamlaka hiyo imesema kwa saa 24 zijazo kuanzia Machi 6 saa 3:00 usiku hadi Machi 7 saa 3:00 usiku, maeneo mengi nchini yanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua, ngurumo za radi pamoja na mawingu.
Open Online Media itaendelea kukuletea taarifa za hali ya hewa na tahadhari muhimu kwa wananchi. Tuachie maoni yako.
#pakua app ya Open Media kupata habari na kusikiliza Open Online Radio
#follow, comment na ku like post za Open Online Media ili uwe wa kwanza kupata habari
Palavra-chave: meteorologia pemba








































